Saturday, May 26, 2012

MAONI YANGU KATIKA ENEO LA AJIRA MJADALA WA DIRA LEO



Asasi ya Dira ya Vijana nchini, (TYVA-Tanzania Youth Vision Association) Leo 26 Mei 2012 imefanya mjadala wa vijana hapa Arusha wenye lengo la kukusanya maoni ya vijana ili yaingizwe katika Katiba Mpya ya Tanzania.

Mada ya Mjadala huu inasema kuwa "Vijana na tunayoyataka ndani ya katiba mpya ya Tanzania". Vijana wanatoa maoni yao katika maeneo takribani kumi, ikiwemo, Baraza Huru la Taifa la Vijana, Ajira, Elimu, Afya, Michezo na Utamaduni, Ushiriki wa Vijana, Utawala Bora, Uchumi wa mtu mmoja mmoja, Vijana wenye ulemavu na Diplomasia ya Tanzania.

Kwa kuwa sikuwepo hapo ukumbini wakati mjada unaendelea, na kama kijana ninawajibika pengeni kusema nini maoni yangu. Kwa leo ningependa nitoe maoni yangu katika eneo la Ajira na namna ninavyotaka kama Mtanzania suala la ajira lilindweje na Katiba Mpya tunayoitarajia hivi karibuni. Maoni juu ya maeneo mengine nitaendelea kujatoa katika mijadala ijayo, pia kupitia safu hii. Leo kwa ufupi sana niseme hivi;-

Tatazo lilipo sera yetu ya viwanda ni butu sana katika kusimamia ajira hapa nchini. Nchi haina viwanda vya ndani vya kutosha kuweza kuzalisha ajira nyingi kwa idadi kubwa ya wananchi wa kawaida. Sehemu kubwa ya ajira leo Tanzania ambapo kila mwaka nchi inapokea graduates 700,000 katika soko la Ajira, ambapo wengi wao wanategemea kufanya the so called White Colar Jobs, sehemu kubwa ya wananchi inayobakia ni wale wasiokuwa na ujuzi ama wanaujuzi usiowatosheleza kupata kazi za ofisini.

Hawa ndio ilibidi Viwanda vya uzalishaji viwaajiri.Lakini hatuna viwanda(Semi Processing, Light and Heavy Industries) huku ukosefu wa ajira ukiendelea kuwa juu kwa asilimia 11 na ushehe! Tunataka katiba mpya iilazimishe nchi kuwa na uchumi unaoleweka na utakao leta ajira kwa usawa. Pia kwa kuanzia sera ya Viwanda iangaliwe upya ili iandane na uwiano wa idadi ya nguvu kazi ya Taifa ambayo wengi wao ni vijana ambao ni 65% of labour force ambayo hata hivyo haitumiki yote kwa kuwa Ajira hamna!